Jumatano, 19 Novemba 2014

WEKA HAZINA YAKO MBINGUNI SIO DUNIANI


WATU WENGI HUMUACHA MUNGU NA KUANZA KUJILIMBIKIZIA HADHINA NYINGI DUNIANI KWASABABU WAPO KUUTAFUTA UTAJILI WA NAFSI NA MWILI NA SIO UTAJIRI WA ROHO ,UTAJIRI WA ROHO HAUCHAKAI WALA HAUFIRISIKI WALA AUIBIWI BALI HUDUMU MILELE NA MILELE
UKIMTUMANI MUNGU KWA MOYO WAKO WOTE NA UKIMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI HUPUNGUKIWI NA KITU KATIKA MAHITAJI TAKO MAANA BIBLIA INASEMA NI NIMEJIFUNZA KUWA NACHO AMA KUPUNGUKIWA LAKINI NINAYAWEZA YOTE KATK YEYE ANITIAE NGUVU
NDUGU MTUMISHI UNAHITAJI KUWA NA MTIZAMO MMOJA ,ILI UWE NA NIA MOJA,KUHUSINA NA NENO LA MUNGU NI LAZIMA ULIKUBALI NENO LA MUNGU KUWA NDIO MAMLAKA YA MWISHO KILE LINACHOSEMA NDICHO LINACHOMAANISHA
WATU WENGI HUTAFUTA PESA SIKU SITA KWA MASAA KUMI NANE KILA SIKU LAKINI MUNGU WAMEMTENGEA JUMAPILI TU NAPO KIOGONGOZI WA IBADA AKICHELEWA KUHUBIRI WANATOKA KWENDA NJE KUTAFUTA PESA
MPWNDWA JARIBU MDA UNAOTUMIA KUTAFUTA PESA UNGETUMIA KUJISOGEZA KARIBU NA BWANA UNGETUMIA KUMTAFUTA MUNGU
MPENDWA PETRO ALIMUULIZA YESU ITAKUWAJE KWA SISI TULIOKUBALI KUACHA KAZI ZETU NA KUKUFUATA WEWE YESU AKAJIBU KWANZA UFALME WA MBINGUNI NI WENU PILI HAMTAPUNGUKIWA NA CHOCHOTE KTKA MAHITAJI YENU
SINA MAANA HUACHE KAZI ULIOAJIRIWA BALI NAAMANISHA ASUBUHI OMBA UPO OFISI OMBA UPO NJIANI OMBA UPO KWENYE BASI OMBA MAANA AJALI NYINGI OMBA MUNGU AKUEPUSHE NA AJALI ILI UWEZE KUMTUMIKIA KWA MDA MWINGI KAMA WATUMISHI WAKE IBRAHIMU MUSA JUA KUWA DHAMBI HUPUNGUZA UMRI WAKO WA KUISHI BALI UKIMCHA BWANA UMRI WAKO WA KUISHI UONGEZEKA
MATHAYO 6:19:23
MSIJIWEKEE HADHINA DUNIANI,NONDO NA KUTU VIHARIBUPO ,NA WEZI HUVUNJA NA KUIBA BALI JUWEKEENI HAZINA MBINGUNI ,KUSIKOHARIBIKA KITU KWA NONDO WALA KUTU WALA WEVI HAWAVUNJI WALA HAWAIBI ;KWA KUWA HAZINA YAKO ILIPO,NDIPO UTAKAPOKUWAPO MOYO WAKO TAA YA MWILI NI JICHO ,BASI JICHO LIKIWA SAFI ,MWILI WAKO WOTE UTAKUWA NA NURU,LAKINI JICHO LIKIWA BOVU,MWILI WAKO WOTE UTAKUWA NA GIZA ,BASI ILE NURU ILIYOMO NDANI YAKO IKIWA GIZA ;SI GIZA HILO !
MSTARI WA 24 YESU ANASEMA HUWEZI KUTUMIKIA MABWANA WAWILI KWA WAKATI MMOJA LAZIMA HUTASONGWA NA BWANA MMOJA
NIMEJIFUNZA KITU KUNA WATUMISHI WA MUNGU WALIOMPA MUNGU MDA WAO WOTE WAMEFANIKIWA SANA KUI
LIKO WALE WALIOIPA FEDHA MDA WAO WOTE AMA WALE WALIOIPA FEDHA NUSU MUNGU NUSU MUNGU AMEWASIKIA SANA WALE WALIOTENGA MDA WAO WOTE KUMTUMIKIA WATAKATIFU MNAWAITA FREE MASON WAKATI FREEMASON NI WEW MWENYE WASIWASI NA MUNGU USIEKIRI JINA USIEJUA YESU NI BWANA KWA ULIMI NA MATENDO
1TIMOTHEO 6:17-19
WALIO MATAJIRI WA ULIMWENGU WA SASA UWAAGIZE WASIJIVUNE,WALA WASIUTUMANIE UTAJIRI WAO USIO YAKINI,BALI WAMTUMAINI MUNGU ATUPAYE VITU VYOTE KWA WINGI ILI TUVITUMIE KWA FURAHA.WATENDE MEMA,WAWE MATAJIRI KWA KUTENDA MEMA WAWE TAYARI KUTOA MALI ZAO ,WASHILIKIANE NA WENGINE KWA MOYO;HUKU WAKIJIWEKEA AKIBA IWE MSINGI MZURI KWA WAKATI UJAO ,ILI WAPATE UZIMA ULIO KWELI KWELI".WAAMBIENI MATAJIRI DUNIA HII KWAMBA WASIJIVUNE,WALA WASIOUTUMANIE UTAJIRI WAO USIO YAKINI".
JIULIZE MTUMISHI MATAJIRI UNAOWAJUA WANATENDA MEMA WANA MPENDEZA MUNGU UKIPATA JIBU TAFAKARI JE MATAJIRI WA SIKU IZI WANASHILIKIANA NA WATU NA HAWAJIVUNI ? TAFAKARI ANGALIA JINSI KANISANI MNAVYOSHILIKIANA
NAKUSIHI USIMWACHE MUNGU KAMA TAYARI UPO NAE NA KAMA UPO MBALI NAE MTAFUTE NA UMSOGEZE KARIBU NA HUISHI NAE MILELE NA UMTUMIKIE KWA MOYO NA UHAMINIFU NA UMWABUDU KTK ROHO NA KWELI
HILI NDILO SOMO LANGU LA IJUMAA HII NIMETOA KWA WALE WASIOABUDU PAMOJA NAMI
KWA USHAURI MAOMBI NA KUKUONGOZA SARA YA TOBA
PIGA 0653543333
0786250359
MUHUBIRI EMANUEL ANDREW MWAKYEJA

Tafakari

TAFAKARI KWA MAKINI MANENO HAYA NA YAWEKE KIFUANI KWAKO YASIKUPITE

HAPO USISEME MOYONI MWAKO ,NGUVU ZANGU NA UWEZO NA UWEZO WA MKONO WANGU NDIO ULIONIPATIA UTAJIRI HUO .BALI UTAMKUMBUKA BWANA MUNGU WAKO MAANA NDIE AKUPAE NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI:ILI ALIFANYE IMARA AGANO ALILOWAPA BABA ZAKO,KAMA HIVI LEO.
WENGI MNAJUA UTAJIRI NI JUHUDI ZENU NA NGUVU ZENU KUMBE MUNGU WA BABA ZETU NDIE ATUPAE INA MAANA ANAWEZA KUKUNYANG'ANYA USIPO MTII NA KUMWABUDU KATIKA ROHO KWELI

SI KWA HAKI YAKO ,WALA KWA UNYOOFU WA MOYO WAKO ,HIVI UINGIAVYO KUIMILIKI NCHI YAO ;LAKINI NI KWA UOVU WA MATAIFA HAYA BWANA MUNGU WAKO AWAFUKUZE NJE MBELE YAKO TENA APATE KULIWEKA IMARA HILO NENO BWANA ALILOWAAPIA BABA ZAKO IBRAHIMU ISAKA NA YAKOBO .BASI JUA YA KUWA BWANA MUNGU WAKO HAKUPI NCHII NZURI UIMILIKI KWA AJILI YA HAKI YAKO ,KWA MAANA UTAIFA LENYE SHINGO NGUMU

KUMBE KULINGIA MAFANIKIO YAKO BILA KUMSIFU MUNGU NI KUJIDANGANYA KUMCHEKA MASKINI NI KUKUFURU
BASI SIFUNI JINA LAKE UTUKUFU NA BARAKA ZISHUKE BILA KUKOMA

Ijumaa, 14 Novemba 2014

Nishike mkono

Nishike mkono ee mungu wangu nipo katikati ya watesi wanaitaka roho yangu
Maadui wananiombea mauti bila ya kujua kuwa mauti ni faida kwangu
Ee mungu ulie juu naikabidhi jumamosi yangu mikononi mwako nauibariki uifanye siku ya mafanikio katika maisha yangu
Baba mungu naileta nchi ya tanzania mikononi mwako ifanye mahala salama pa kuishi uipake mafuta uipe neema mbele ya mataifa
Baba mungu katika jina la xesu kristo nawaleta kwako wagonjwa wagumba tasa wenye shida na mateso mbali mbali na waliofungwa na hila za muovu waliokamatwa na shetani kuanzia sasa nawatangazi uhuru wa mateso yao ukawakumbatie ewe mfariji wa wawafaruji maana wewe ndio.msaada wakp
Wanakuinulia macho yao ili wakuone bwana onekana mbele zao
Isayah 41:10
USIOGOPE KWA MAANA MIMI NI PAMOJA NAWE USIFADHAIE KWA MAANA MIMI NI MUNGU WAKO NITAKUTIA NGUVU NAAM NITAKUSAIDIA NAAM NITAKUSHIKA KWA MKONO KUUME WA HAKI YANGU
KILA GUMU MSAADA NI MUNGU
KILA JARIBU LAKUPASA KUSHINDA TUOMBEANE TUSIWEKEANE UNABII MAANA HAKUNA MKAMILIFU
YESU MWANA WA MUNGU NITAZE KAMA ULIVOMTIZAMA SAULI NIPE MAONO ANGAVU  NISAIDIE VITA YANGU IMEKUWA NA MIIBA NA MOTO MKALI NIFANYE JESHI IMARA ILI ULIMWENGU UTAMBUE THAMANI YA KIFO CHAKO

Alhamisi, 13 Novemba 2014

Busara zamungu

NAMI NIMEZITUMAINI FADHILI ZAKO MOYO WANGU NA UFURAHIE WOKOVU WAKO

ONJENI MUONE BWANA YUMWEMA ,HERI MTU YULE ANAYEMTUMAINI

EWE MUNGU JINSI ZILIVYO NA THAMANI FADHILI ZAKO ,WANADAMU HUKIMBILIA UVULI  WA MBAWA ZAKO

MAANA NDIWE TARAJA LANGU EE BWANA MUNGU TUMAINI LANGU TOKEA UJANA WANGU

MOYO WANGU NA MWILI WANGU VINAMLILIA YEYE ALIYEHAI

BALI MIMI NI KAMA MZEITUNI UMEAO KATIKA NYUMBA YA MUNGU NAZITAMANI FADHILI ZA MUNGU MILELE NA MILELE

MTUMAINI BWANA KWA MOYO WAKO WOTE WALA USITEGEMEE AKILI ZAKO MWENYEWE 
KATIKA NJIA ZAKO ZOTE MKIRI YEYE ,NAYE ATANYOOSHA MAPITO YAKO

KUMCHA BWANA NI TUMAINI IMARA
ATAKAERITAFAKARI NENO ATAPATA MEMA NA KILA AMWAMINIYE BWANA  ANA HERI

TAZAMA MUNGU NDIYE WOKOVU WANGU NITATUMAINI WALA SITAOGOPA MAANA BWANA YEHOVA NI NGUVU ZANGU NA WIMBO WANGU NAYE AMEKUWA WOKOVU

MTUMAINI BWANA SIKU ZOTE MAANA BWANA  YEHOVA NI MWAMBA WA MILELE

AMEBARIKIWA MTU YULE AMBAYE BWANA NI TUMAINI LAKE

MAANA NAYAJUA MAWAZO NINAYOWAWAZIA NINYI ASEMA BWANA NI MAWAZO YA AMANI WALA SI YA MABAYA KUWAPA NINYI TUMAINI SIKU ZENU ZA MWISHO

Mwanadamu hakujiumba bali aliumbwa
Na kama aliumba basi sifa na utukufu zirudi kwake
Mungu wetu ni mwenye huruma mara zote utuwazia mema na neema
Asante yesu kufa kwako ni uhai wangu na ondoleo la dhambi zangu

Usiyumbe wala kutishwa yesu yu nawe katika majaribu yako

Watumishi wengi wa mungu huondolewa imani yao juu ya kristo kwa sababu ya maneno ya mataifa au maneno ya watishi wenza waumini, au wapinga kristo
Mtumishi yeyote wa mungu lazima uwe na moyo uliothibitika na agano lililothibitika juu ya yesu kristo pasi na shaka yoyote  na huku ukimfanya mungu mamlaka ya mwisho kwa kila jambo ndani ya maisha yako
Mungu haisaidiwi wala hapimwi maana yeye ni msaada tosha juu ya maisha yako na kipimo stahiki juu ya matendo yako
Watumishi wengi huanguka kiimani kwasababu ya kiburi na na kukosa imani yenye ujasiri ndani yake iliyojaa uweza wa roho wa mtakatiifu
Imani pasipo ujasiri na matendo mema si kitu mbele za muovu ili uweze kumshinda muovu lazima uthibitike na uthibitishwe na uwe jadiri bila kurudi nyuma

WAFILIPI 1:20;21
20 KAMA VILE NILIVYOTAZAMIWA SANA NA KUTUMAINI KWAMBA SITAAIBIKA KAMWE BALI KWA UTHABITI WOTE KAMA SIKU ZOTE NA SASA  VIVYO HIVYO KRISTO ATAADHIMISHWA KATIKA MWILI WANGU IKIWA KWA MAISHA,YANGU AU IKIWA KWA MAUTI YANGU
21 KWA MAANA KWANGU MIMI KUISHI NI KRISTO NA KUFA NI FAIDA

2TIMOTHEO 3:10-15
10 BALI WEWE UMEYAFUATA MAFUNDISHO YANGU NA MWENENDO WANGU NA MAKUSUDI YANGU MA IMANI YANGU NA UVUMILIVU WANGU
11 NA UPENDO NA SABURI TENA NA ADHA ZANGU NA MATESO YANGU MAMBO YALIYONIPATA KATIKA ANTOKIO KATIKA IKONIO NA KATIKA LISTRA KILA NAMNA YA ADHA NILIYOISTAIMILI NAYE BWANA ALINIOKOA YOTE KATIKA HAYO YOTE
13 LAKINI WATU WABAYA NA WADANGANYAJI WATAENDELEA NA KUZIDI KUWA,WAOVU WAKIDANGANYA NA KUDANGANYIKA
14 BALI WEWE UKAE KATIKA MAMBO YALE ULIOFUNDISHWA NA KUHAKIKISHWA KWA MAANA UNAJUA NI AKINA NANI UNAOJIFUNZA KWAO
15 NA YA KUWA TANGU UTOTO UMEYAJUA MAANDIKO MAANDIKO MATATIIFU AMBAYO YANAWEZA KUKUHEKEMISHA HATA UPATE WOKOVU KWA IMANI ULIYO KATIKA YESU KRISTI

YAKOBO 1:2-4

NDUGU ZANGU HESSABUNI YA KUWA NI ,FURAHA TUPU MKIANGUKIA KATIKA MAJARIBU MBALIMBALI
3 MKIFAHAMU YA KUWA KUJALIBIWA KWENU KWA INANI YENU HULETA SABURI
4 SABURI  NA IWE KAZI KAMILIFU MPATE KUWA WAKAMILIFU NA WATIMILIFU BILA,KUPUNGUKIWA NA NENO
5 LAKINI MTU AKIPUNGUKIWA NA HEKIMA NA AOMBE DUWA KWA MUNGU AWAPAYE WOZE KWA UKARIMU WALA KAMEI .NAYE ATAPEWA

6 ILA AOMBE KWA IMANI PASIPO NA SHAKA YOYOTE MAANA MWENYE,SHAKA NI KAMA WIMBI LA BAHARI LILILICHUKULIWA JA UPEPO NA KUPEPERUSHWA HUKU NA HUKU

1PETRO 4:12-13
WAPENZI MSIOONE KUWA NU AJABU ULE MSIBA ULIO KATI YENU UNAOWAPATA KAMA MOTO ILI KUWAJARIBU KANA KWAMBA NI KITU KIGENI KIWAPATACHO
13 LAKINI KAMA MNAVYOSHILIKI MATESO YA KRISTO FURAINI ILI NA  KATIKA UFUNUO WA UTUJUFU WAKE MFURAHI KWA,SHANGWE

UVUMILIVU NA MAOMBI BILA,KUKOMA  NDIO NGUZO YETU YA KUTUFANYA,TUBAKI  IMARA KATIKA IMANI YETU JUU YA BWANA WETU YESU KRISTO
YEYE NI BABA
IMEANDALIWA NA MUHUBIRI EMANUEL ANDULILE MWAKYEJA
0653543333
0786250359
YU MWEMA

Jumatano, 12 Novemba 2014

Sara ya wokovu

Baba wa mbinguni ninakuja kwako katika jina la yesu neno linasema yeyote atakaeliita jina la bwana ataokoka matendo ya mitume 2:21.ninakuita wewe bwana yesu.ninakuomba ewe yesu uingie ndani ya moyo wangu  na kufanyika bwana juu ya maisha yangu kulingana na warumi 10:9-10
Kwasabu ukimkiri yesu kwa kinywa,chako ya kuwa ni bwana na kuamini kuwa mungu alimfufu katika,wadu utaokoka maana moyo wa mtu huamini na kupata haki na hukiri na kupata wokovu
SAsa nimezaliwa upya mimi ni mkristo  mtoto wa mungu alie hai nimeikoka
Pia nakuomba unijaze roho mtakatifu roho wa mungu furika ndani ya moyo wangu
Ninatarajia kwa moyo wote kunena kwa lugha kwa uweza wa roho mtakatiifu
Sema amen

Jumatatu, 22 Septemba 2014

HAKI ZA BINADAMU ???


By Apostle eliya simon-
KUTUMIA UHURU KUWA HURU.

YALIYOMO
  1. Utangulizi
  2. Uhuru wa Hiyari
  3. Madhara ya Uhuru
  4. Hitimisho
ANDIKO KUU: Kumbu Torati 30:15-20
….nimekuwekea mbele yako leo uzima na mauti, Baraka na laana….
LENGO LA SOMO:
            i.Ni kuonyesha uhuru wa kuwa huru   
                (ii). Kufichua kichaka cha Haki za Binadam
1.UTANGULIZI
•►Haki za binadamu,ni msemo ambao upo mdomoni mwa watu na taasisi nyingi, umoja wa mataifa wanakazia haki za binadamu,serikali na taasisi zake, mashirika na mtu binafsi-binafsi wamekuwa macho kwenye haki za binadamu
►Kuna nini hasa nyuma ya haki za binadamu? Kuna ajenda gani ya siri inayoendelea?
Katika fundisho hili la haki za binadamu,utajifunza maneno yanayoambatana na haki za binadamu,kama UHURU, HIYARI NA MAAMUZI, pia utajifunza kutumia uhuru wako kutokuwa huru.
2.UHURU WA HIYARI
-►Linapotumika neno HAKI ZA BINADAMU, UHURU, HIYARI, maneno haya ni kama kivuri au kichaka kinachoficha uhalisia wa nia ya moyoni. Nia ya moyo wa mwanadamu toka enzi na enzi ni kutaka kutumia uhuru kuwa huru, mbali na Mungu na sheria na amri zake,hitaji hili la moyo linajificha ndani ya HAKI ZA BINADAMU na UHURU WA HIYARI.
-►Uhuru wa hiyari ndio jambo la pekee ambalo mwanadamu amepewa na Mungu uhuru asilimia 100, Mungu hana haki ya kuvunja uhuru wa hiyari wa mwanadamu hata nukta moja. Kwa uhuru wa hiyari alionao Mwanadamu, maamuzi yapo mikononi mwake. Kuwa na uhuru sio dhambi,lakini kutumia uhuru ili kuwa huru ndio dhambi.
A) UHURU WA HIYARI YA MAAMUZI TUMEPATA WAPI?
►Tunafahamu kuwa mwanadamu wa kwanza ni Adam na Eva, kabla ya kuasi kwao uhuru wa hiyari zao zote walimkabidhi Mungu, hivyo walitumia uhuru wao kutokuwa huru,lakini siku walipoamua kutumia uhuru wao kuwa huru ndipo walipoharibu.
- Mwanzo 3:1-7, Shetani kabla hajawa shetani, alikuwa malaika, lakini baadae akatumia uhuru wake kuwa huru, awe mbali na Mungu. Eva nae akachagua kuwa HURU mbali na Mungu na Adamu nae akawa ndani ya mstari. Toka mwanadamu wa kwanza alipochagua kutumia uhuru wake kuwa HURU mbali na Mungu, ndio wote tukapata uhuru wa hiyari.
B) KWANINI UHURU?
►Kuna sababu zinazomfanya mwanadamu atake kuwa huru, na hizi sababu zimejificha nyuma ya neno HAKI ZA BINADAM na neno UHURU,toka Adamu alipoasi kwasababu ya kutaka kuwa huru na ndio mpaka leo dhambi kubwa ya wanadamu ni kutaka uhuru wao kuwa huru, mbali na Mungu na sheria zake na amri zake.
► Mambo matano(5) yanayomdanganya mwanadamu kutaka kutumia uhuru wake kuwa huru bila Mungu: Maarifa, Pesa, Dini, Tamaduni, Serikali. Haya mambo 5 ambayo ninayaita M’BADALA WA UFALME siyo mabaya wala sio dhambi isipokuwa namna yanavyotafutwa kwa kudhaniwa kuwa kuna uhuru ndio tatizo.
MAARIFA
►Mwanadamu anadhani kuwa siku atakapopata maarifa ya kutosha atakuwa huru,tena atajitoshereza mahitaji yake mbali na Mungu. Hii dhambi ndio ya Adamu na Eva hasa, ule mti ulikuwa unafaa kwa maarifa, neno maarifa limetokana na neno la kilatini (sciencia) likimaanisha sayansi(elimu).
► Nenda chuo chochote muulize mwanachuo mmoja kwanini anatafuta sana maarifa,atakupa majibu mazuri ambayo hayataonyesha waziwazi kuwa anataka kuwa huru mbali na Mungu,ndio maana nikasema hii dhambi niya moyoni zaidi. Kwanini elimu imepewa kipaumbele sana kuliko ufalme wa Mungu? Tatizo nini? …. Uhuru.
PESA, DINI, TAMADUNI NA SERIKALI
► Kwakifupi,mambo yote ambayo mwanadamu anadhani kuwa niya muhimu sana kuliko Mungu, ni kumkataa Mungu na kutaka kuwa huru kwa jina halali la pesa,dini,tamaduni na serikali. Kitendo cha kutafuta sana haya mambo 5 n’nje ya Mungu ni sawa na kumwambia Mungu unataka ujiendeshe mwenyewe asikuchoshe na amri zake.
3.MADHARA YA UHURU
► Toka Adamu, moyo wa mwanadamu unamchukia Mungu, hivyo huwa unatafuta njia m’badala wa kumtoa Mungu katika maisha ya mwanadamu,kama nilivyosema hapo juu,m’badala ambao mwanadamu amejitafutia ni yale mambo 5 hapo juu. Haki za binadamu zinajaribu kumwambia mtu atumie uhuru wake kuwa huru na Biblia (Mungu)
-JUHUDI ZA KUTUMIA UHURU KUWA HURU
A) ADAMU-Mwanzo 3:23-24
► Shetani alitumia uhuru wake kuwa huru mbali na Mungu,akafukuzwa mbinguni, Adamu na Eva walitumia uhuru wao kuwa huru mbali na Mungu,wakafukuzwa Edeni.
Haya ndio matokeo ya kutumia uhuru wa hiyari kuwa huru, kila maamuzi anayoyafanya mwanadamu, Mungu atahakikisha mwanadamu anapata matokeo ya maamuzi yake.
B) WANA WA ISRAELI NA MUSA –Hesabu 14:26-28
► Moyoni mwa wana Israeli hawakumtaka Mungu wa mababa zao,ambae Musa alimtambulisha kwao, sasa ili wawe huru na miungu yao ya Misri, wakataka kurudi Misri kwa kisingizio cha njaa, vita , kifo na magonjwa. Baada ya Musa kuwa mlimani kwa siku 40 ndipo wakaonyesha kilichokuwa moyoni,waliabudu sanamu.
►Utagundua dhambi ya uhuru siku zote huwa inajaribu kujificha kwenye jambo ambalo litaonekana kuwa halali, uhalali ukishapatika ndipo utakapogundua kilichokuwa nyuma ya uhuru. Mpaka sasa ni nani asiyejua umuhimu wa elimu na pesa? Hizi ni sababu halali
C)  ISRAELI NA SAMWELI —1 Samweli 8:4-7
► Ile dhambi ya kutaka kuwa huru haikuishia jangwani kwa Musa, ikaendelea mpaka wakati wa Samweli. Kutaka mfalme ilikuwa ni kisingizio tu,lakini dhumuni hasa ilikuwa ni kuwa huru mbali na Mungu waliyedhani anamashariti na masheria mengi. Mungu akawapa walichokitaka na matokeo ya maamuzi yao akawabebesha.
► Baadhi ya madhara ya maamuzi yao mpaka leo tunayaona hata hapa Tanzania, kodi,ushuru, ajira kuwa serikalini, maisha kuwa juu ili viongozi walipwe. Yote haya ni matokeo ya Mwanadamu kutaka kuwa huru mbali na Mungu kwa kisingizio cha kutaka Raisi na serikali isiyofungamana na dini yoyote. Serikali haina dini? Kwanini?
D) WANA WA ISRAELI NA YESU – Yohana 8:21-23
►Toka kwa Adam, wakati wa Musa,na wakati wa Samweli mpaka nyakati za Yesu kale kamchezo ka mwanadamu kutaka kuwa huru bado kalikuwa kanamkeleketa moyoni. Wakamkataa Yesu kwa njia halali ya Uhuru na Haki ya mwanadamu ya kuchagua.
E) NYAKATI ZETU
►Nyakati hizi niza wasomi wengi, lakini ile dhambi ya kutaka kutumia uhuru kuwa huru bado ipo moyoni, ingawa dhambi ni ileile lakini miaka hii imetengenezewa mazingira na majina mazuri (Haki za Binadamu), na nyimbo zimetungwa – Freedom Song, na filamu zimetengenezwa – Independent Day, na vyuo vimejengwa – Liberty University, na Luninga hazipo mbali – Independence Television(ITV), Na nyimbo za Taifa(Anthem)--♫...dumisha uhuru na umoja…♫,pia …♫.utumwa wa nchi nyerere ameukomesha…♫
4.HITIMISHO
►Wana siasa na watu mbalimbali wanapopigania haki za binadamu, usidhani ya kwamba wanauzalendo sana, hapana,wana ajenda yao ya siri,ipi hiyo? Wanataka utumie uhuru wako uwe huru katika maamuzi yako bila kuingiliwa na misingi ya Mungu na Biblia
► Ungeniambia nikushauri, ningekushauri mambo mawili ;
            i) Usitumie uhuru wako kuwa huru, na 
            (ii) Tumia uhuru wako kutokuwa huru.
    .......HOSE………THE BEST HAS COME………….

KUWA ROHONI

Apostle Eliya Simon 0717 267676

KUWA ROHONI?
Kuwa Rohoni ni kuwa na Daiolojia na Mungu. Daiolojia ni mazungumzo baina ya pande mbili, nikimaanisha Mungu na Mwanadamu. Tuangalie daiolojia Agano la Kale na Jipya.
A. AGANO LA KALE
Agano la Kale Mungu alizungumza na Wanadamu kwa njia mbalimbali, Mgawanyo wangu wa daiolojia na Mungu nimeugawanya kwa kuzingatia idadi ya wahusika.
1. Moja kwa moja na mtu binafsi (wachache)
a. Ndoto – Danieli 2:19
b. Maono – Ezekieli 1:1
c.Ana kwa ana – Kutoka 33:11, Hesabu 12:7-8
2. Kupitia Mtu mwingine(wengi)
a. Kuhani (Urim, Thumimu na Naivera) – Kutoka 28:30-31,1 Samweli 28:6
b. Unabii – Kumbu Torati 18:18
3. Kupitia Kitu(Kiumbe) kingine
a. Punda – Hesabu 22:28
b. Samaki – Yona 2:10
c.Kiganja – Danieli 5:5-6
d. Malaika – Kutoka 33:2a
B. AGANO JIPYA
Agano Jipya Mungu ameboresha Daiolojia, ni kinyume cha Agano la Kale. Lakini bahati mbay wahusika wa Agano Jipya hawapo makini ukilinganisha na wale wa Agano la Kale.
1. Moja kwa moja na Mtu binafsi (wengi)
a. Yesu – Ebrania 1:1-2
b. Roho Mtakatifu – Ufunuo 2:7, Matendo 13:2
c. Kuwa Rohoni – Ufunuo 1:10
2. Kupitia Mtu mwingine(wachache)
a. Nabii – Matendo 11:27-28
b. Malaika – Matendo 10:3-4
C. KIZAZI  KIPYA -- Zaburi 24:6
-Pamoja na njia zote nilizozitaja hapo juu,bado Mungu anaweza akazungumza na Mwanadamu kwa njia yoyoyte na kaktumia chochote. Mungu hana mipaka, vitu vyote ni watumishi wake.
Njia zote za Mwanadamu kuongea na Mungu au Mungu kuongea na Mwanadamu ni nzuri lakini iliyo bora kuliko zote ni kuongea kwa kupitia Yesu kwa njia ya Roho Mtakatifu, wewe utatakiwa kuwa rohoni ili uwe na Daiolojia.
Ungependa kuwa rohoni?
........HOSE.........................THE BEST HAS COME............