AINA YA MIFUNGO
Mpendwa wangu jana tuliangalia utangulizi wa kwanini tunafunga na aina ngapi za maombi. Leo tuziangalie hizo aina za mifungo na kwann tunafunga .
Kwanini tunafunga?
Kwa ujumla Tunafunga ili:
• Kuna watu wanafunga kwa sababu za kimwili kabisa. Kwamba miili yao imefika wakati inawapa shida. Matamanio ya mwili yameshindwa kuwasiliana vizuri na roho. Kuna nyakati tamaa za mwili zinakuwa kubwa na hivyo kwa kufunga na kuomba waweza kuutiisha mwili huu. Kwa vijana hasa, vyakula na vinywaji tunavyokula vinaleta shida wakati mwingine ndani ya mwili. Kwa kufunga unautiisha mwili na kuzinyamazisha tamaa hizo. Wengine wanafunga kwa ajili ya kuyatiisha mawazo. Bwana Yesu akasema mawazo ndiyo yamtiayo mtu unajisi. Kabla mtu hajafanya uasi Fulani huanza kujichafua katika mawazo yake. Ndani ya mawazo yake ataua, atamtukana mtu, atazini, ataiba yani atafanya kila lililo baya kabla hajalifanya katika ulimwengu wa kimwili. Rafiki yangu mmoja akasema ikiwa mwanadamu anaweza kupangilia mipango mbali mbali miovu hadi akaitimiza kwa nn asiweze kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya Mungu? Kwa hyo wakati mwingine mtu anafunga kuyatiisha mawazo machafu ndani yake. Mawazo machafu hututia unajisi! Ndo maana mtume Paulo akasema “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu” 2Kor 7:1
• Lakini kiroho tunafunga ili kuweka mahusiano yetu na Mungu vizuri rohoni. Ezra 8:21-23
“Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote. Maana naliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao. Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali”
Kiundani:
1. Kusudi kuu ni kuutafuta uso wa Mungu katika kile tunachokiomba 2Nyak 7:14
2. Kujinyenyekeza mbele za Mungu “Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu”- Zab. 35:13
3. Kupata usikivu toka kwa Mungu Isaya 58:9 “Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu”
4. Toba kwa ajili ya mtu binafsi, Kanisa, au Taifa. Mfano: 1 Sam. 7:6 Nehemia 9:1-3
5. Maombolezo (Ezra 10:6) Daniel 10:2-3
6. Kutafuta ulinzi na uongozi wa Mungu katika mambo Fulani Fulani 2Nyak. 20:3 “Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote" waweza pia kuangalia Ezra 8:21-23 kama tulivyoona hapo juu. Mdo 14:23 “Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.” Neh 1:4 “hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni”
7. Kama sehemu ya kumwabudu Mungu (Waamuzi 20:26, (Neh 9:1-3) (Luka 2:36-37)
8. Kwa ajili ya maombezi (Isaya 58:6-7, Daniel 6:18)
9. Kufanya ukombozi kwa ajili ya utumwa wa kiroho (Isaya 58:6, Mathayo 17:18-21)
10. Kujiandaa kwa ajili ya huduma maalumu (Mathayo 4:1-2, (Luka 4:1-2, Mdo 13:2-3
11. Kurudisha afya ya mtu (ISaya 58:8-11)
12. Kuimarisha ndoa (1 Kor 7:5)
Aina ya mifungo:
1. Mfungo kamili
Katika mfungo huu hakuna kula kabisa chakula kigumu bali waweza kunywa maji au kimiminika chochote cha kukusupport.
Siku ngapi waweza kufunga mfungo wa aina hii unategemea na neema na malengo yako katika mfungo huo. Wengine huenda siku moja, mbili, tatu, wiki, n.k n.k
2. Mfungo nusu
Mfungo nusu huanzia saa 12 asbh hadi saa 9 mchana au kuanzia jua linapoibuka hadi linapozama. Mfungo ambao madhehebu mengine wamewazoeza waumini wao kuufanya. Wengine wameweza kuufanya kila ijumaa. Madhehebu ambayo yamewazoesha watu wao kufunga angalau kila wiki mara moja wameweza kuwa na mafanikio makubwa sana katika kuzifungua nira na vifungo mbali mbali
3. Mfungo wa Daniel
Daniel alifunga mifungo miwili ya aina yake;
• Katika Sura ya I Daniel alifunga alikula mboga mboga tu (Yaweza kuwa alikula mboga mboga na juisi Fulani Fulani)
• Katika sura ya 10 Daniel alifunga kwa siku 21 kwa kutokula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwake”
Tutaendelea na Mungu akubariki. Ukiwa una jambo lolote unataka kutushirikisha tuombe pamoja nawe basi wasiliana nami
0653543333
Andulileemanuel@gmail.com
Au soma katika blog
www.tukofarini.blogsport.com
Jumanne, 14 Aprili 2015
Mifungo
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni